Saltar al contenido

Watasema sana

por Samson Madawabora

Unaweza kushangaa “mi amor” maana yake nini,
Mi amor maana yake ni mpenzi wangu,
Au kwa lugha ya kiingereza ni “my love”
“Mi amor” ni lugha ya Uhispania.
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Kwa kawaida huwa natumia lugha nne.
Ninapokuwa naandika barua kama hii,
Au jambo linalohusu mapenzi ya dhati,
Samahani mi amor kwa kukupa neno jipya,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Vipi maisha hapo ulipo mpenzi wangu?
Nahisi umzima wa afya kabisa,
Lakini siwezi kuhakikisha kabisa,
Mpaka wewe mwenyewe úseme kabisa,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Kama umzizma na unalijua lilipo kanisa,
Wewe ndiye unayejua ukweli wote kabisa,
Nitafurahi kusikia kuwa umzima kabisa,
Nikipata majibu yako kwa muda muafaka kabisa,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Ni safari ndefu ya mwanadamu kimaisha na mapenzi,
Iwe mke au mume mara moja kubahatika,
Maishani mwake kumpata mtui fulani,
Ambaye ni maalumu sana kwake,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Kwa kiasi kikubwa nimetambua na kuamini,
Kuwa kukutana kwetu ni mwanzo wa kutimia,
Kwa ile ndoto yangu ya siku nyingi:
Ya kumpata mwenzi wangu wa maisha,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Kila siku maishani mwangu nilkuwa ana ndoto:
Ya kumpata mwenzi wangu wa maisha,
Nifunge naye pingu za maisha tuwe pamoja,
Nimekuchagua wewe uwe wangu wa maisha
ya kufa na kuzikana,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Usijali maneno mengi watu wasemayo,
Yaliyopita si ndwele,tugange yanayokuja,
Maana nimekuchagua wewe uwe wangu,
Wangu wa maisha ya kufa an kuzikana,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Nakupenda wewe malaika wa moyo wangu,
Nakuhusudu wew ua la moyo wangu,
Nakupenda sana “mi amor” wangu,
Moyo nina furaha tele uko mikononi mwangu,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Na kwa pete hii ninakuoa uwe wangu,
Mke wangu wa ndoa,daima nakupenda,
Hakika wewe ni ubavu wangu wa dhati,
Kama meli imetia nanga kwako kwingine
katu sintotamani,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Umewaacha wazazi wako baba na mama,
Kwa mapenzi umeungana nami katika
ndoa Takatifu,
Na leo hii si wawili tena,tu mwili mmoja,
Tumwombe Mungu atujalie ndoa yenye Baraka,
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Tuje tuzae na watoto waizunguke meza yetu,
Upendo utawale nyumba yetu siku zote daima,
Tuwe wakarimu kwa wageni wetu wote,
Maana nimekuchagua wewe uwe wangu
wa maisha.
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.

Mpenzi nimeona wengi wewe umewashinda wote,
Nakupenda wewe malaika wa moyo wangu,
Nakuhusudu wewe ua la moyo wangu.
Mengi watasema lakini sisi ni hadi milele.
Penzi letu linakuwa kulingana na wakati.